Rais Xi Jinping atuma salamu za pongezi kwa Mkutano wa Amani wa Vijana Duniani

BEIJING – Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za pongezi kwa Mkutano wa Amani wa Vijana Duniani uliofanyika Beijing, mji mkuu wa China jana Jumanne.

Amesema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan, na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, na katika miaka 80 iliyopita, watu wa China pamoja na watu duniani katika kufanya vita vya kumwaga damu na kushinda taabu kubwa sana, waliushinda kabisa ufashisti na kupata amani ambayo si rahisi kupatikana.

Amesisitiza kuwa, matumaini ya mustakabali wa amani ni kwa vijana, na anatumai marafiki vijana kutoka nchi mbalimbali duniani watachukua mkutano huo kama fursa ya kubadilishana maoni, kuongeza maelewano na kujenga urafiki.

Rais Xi amewataka vijana hao wawe watetezi wa wazo la amani, na kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya amani na ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Mkutano huo wenye kaulimbiu ya “Pamoja kwa Amani,” umeandaliwa kwa pamoja na Shirika la Urafiki wa Watu wa China kwa Nchi za Nje na Shirikisho Kuu la Vijana wa China.

滚动至顶部