BEIJING – Xi Jinping, Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametia saini amri ya kutangazwa kwa bendera za kijeshi za aina za vikosi vya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), vikiwemo pamoja na vikosi vya anga ya juu vya kijeshi, vikosi vya nafasi ya mtandao, vikosi vya uungaji mkono wa upashanaji habari na vikosi vya uhakikisho wa ugavi.
Katika wakati wa kuadhimisha Siku ya Tarehe Mosi Agosti ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China, Rais Xi ametoa salamu za sherehe kwa wanajeshi wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Jeshi la Polisi la China, wafanyakazi wa kiraia wanaofanya kazi jeshini, na askari wa vikosi vya akiba na wanamgambo.
Kutangazwa kwa bendera hizo za kijeshi kumeonesha kuanzishwa kwa mfumo wa bendera za kijeshi wa jeshi la umma katika zama mpya, unaojumuisha bendera ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), bendera za jeshi la nchi kavu, jeshi la majini, jeshi la anga, jeshi la roketi, vikosi vya anga ya juu vya kijeshi, vikosi vya nafasi za mtandao, vikosi vya uungaji mkono wa upashanaji habari, na vikosi vya uhakikisho wa ugavi.
Bendera hizo za kijeshi zimeanza kutumika rasmi kuanzia leo Tarehe Mosi, Agosti.
Kamati kuu ya kijeshi imetoa uamuzi wa kurekebisha kanuni zinazofuatwa kwa majaribio kuhusu usimamizi wa bendera za kijeshi, kufanya marekebisho ya kanuni kuhusu aina na matumizi ya bendera za kijeshi mbalimbali ili kusanifisha usimamizi wake na kulinda heshima za bendera za kijeshi kwa mujibu wa uhakikishaji wa utekelezaji kisheria.